Mambo muhimu ya kufahamu wakati unatafuta hati miliki ya kiwanja chako. Kwa mujibu wa sheria mama ya ardhi namba 4 ya 1999 kifungu cha 4 (1) kinaeleza wazi kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya uma na rais ndiye msimamizi au mmiliki kwa niaba ya wananchi wote wa jamhuri ya Tanzania (Sheria ya Ardhi ya Tanzania bara ni tofauti na ile ya Zanzibar). Lakini pia imeweka wazi kuwa mwananchi yeyote wa tanzania...