Hatua na Jinsi ya Kupata Hati Miliki Ya Kiwanja 2022

Mambo muhimu ya kufahamu wakati unatafuta hati miliki ya kiwanja chako. Kwa mujibu wa sheria mama ya ardhi namba 4 ya 1999 kifungu cha 4 (1) kinaeleza wazi kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya uma na rais ndiye msimamizi au mmiliki kwa niaba ya wananchi wote wa jamhuri ya Tanzania (Sheria ya Ardhi ya Tanzania bara ni tofauti na ile ya Zanzibar).

Lakini pia imeweka wazi kuwa mwananchi yeyote wa tanzania hata miliki ardhi moja kwa moja (free hold) bali atapewa haki ya kutumia ardhi kwa muda maalumu kwa kifupi serikali itakukodishia ardhi (leasehold).

Na ndiyo maana hati miliki hutolewa kwa kipindi cha ukomo wa muda fulani mfano hati milikinyingi hutolewa kwa kipindi cha kuanzia miaka 33, 66 na 99, hivyo ikiisha hiyo miaka inatakiwa ukatengeneze hati nyingine.

Hivyo muda wote ukiwa unatumia ardhi unapaswa kufahamu kuwa wewe una haki ya kutumia Ardhi wala si mmliki wa Ardhi kwa kuwa sheria inasema wazi kwamba Ardhi ni mali ya umma (serikali).

Ndiyo maana katika hati miliki yako kumewekwa masharti au matumizi ya ardhi hiyo na ukiyakiuka hayo masharti ardhi yako inachukuliwa na serikali. Hili lipo wazi kwani mara nyingi mashamba au ardhi za watu walioshindwa kuendeleza au kubadilisha matumizi waliyopangiwa hupokwa ardhi hiyo na serikali kwa sababu ndiyo mmiliki wa ardhi yote.

Hivyo basi haki za kutumia ardhi(granted right of occupancy)hupewa kwa mtu ambaye ardhi yake imepimwa tu yani hati miliki kwa mujibu sheria namba 4 ya ardhi ya 1999 ambayo ndo sheria mama ya ardhi tanzania.

kifungu cha 22 (1)(a) na (c) kimesema kuwa hati miliki itatolewa na rais (kwa sababu ndiye msimamizi wa Ardhi kwa niaba ya wananchi) kwenye ardhi ambayo imepimwa tu. Hivyo ili upate hati miliki lazima upime ardhi yako huwezi kupata hati miliki kwenye ardhi ambayo haijapimwa.

Aina Za Hati Miliki

Kuna aina kuu mbili za umiliki ardhi kama unavyotambuliwa na sheria za nchi ambazo ni sharia ya Ardhi namba 4 na namba 5 za 1999.

 1. Umiliki wa ardhi wa kiserikali (granted right of occupancy)
 2. Umiliki wa ardhi wa kimila(customary right of occupancy).

Aina hizi za kumiliki ardhi sio ngeni kwani ndizo zilikuwa zinatumika hata katika Sheria ya Ardhi ya zamani (ya kikoloni n ahata baada ya ukoloni) ambayo ilifutwa na kutungwa sheria za ardhi za mwaka 1999.

Mtu Anaepaswa Kuwa na Hati Miliki Ya Kiwanja ni Yupi?

 1. Mtanzania, mwanamme au mwanamke.
 2. Kikundi cha watu ambao ni raia wa Tanzania walio katika umoja wa kisheria au la, au ni wabia au washirika
 3. Ifahamike kwamba mtu ambaye sio raia wa Tanzania, au kikundi cha watu au mtu ambaye na shirika lenye hisa, ambao wengi wa wanahisa wake sio Watanzania hawana haki ya moja kwa moja ya kumiliki ardhi nchini na kupewa hakimiliki ya ardhi isipokuwa tu kama watapewa ardhi hiyo kama wawekezaji wa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997.

Ili kuweza kupata hati miliki Maeneo ya Mjini.

 1. Eneo husika lazima liwe limetangazwa kuendelezwa kimipango miji(Planning areas).
 2. Eneo liwe limeandaliwa michoro ya Mipango Miji na kusajiliwa wizarani.
 3. Eneo liwe limepimwa kwa kufuata mchoro wa mpango mji uliopo na kupata usajili kwa Ramani hiyo ya upimaji wizarani.

Kwa viwanja Vilivyopimwa

Unapaswa kufahamu kuwa kwa maeneo yaliyokwisha kupimwa aidha na makapuni binafsi yanayosimamiwa na halmashauri ama maeneo yaliyopimwa na halmashauri zenyewe unapaswa kuzingatia hatua zifuatazo ili kupata hati miliki ya kiwanja ama shamba lako lilipo maeneo ya mjini.

 1. Jaza Fomu ya maombi fomu ya maombi ya kumilikishwa kiwanja kiwanja(Land Form Na 19). Amabpo utajaza taarifa zako binafsi ikiwemo majina yako, anuani yako n.k
 2. Ukisha kubaliwa maombi ya kupata kiwanja utatakiwa kulipia gharama ya kiwanja husika (kama kipo chini ya halmshauri husika). amabayo itategemeana na ukubwa na matumizi ya kiwanja.
 3. Baada ya kulipia kiwanja utaandikiwa nyaraka ya Ankara ya malipo ya gharama za HATI (Tittle costs) katika kiwanja chako. Gharama hizi ni pamoja na:
 • Premium fee: Eneo la kwanja x Gharama ya kiwanja kwa mita mraba x 0.025
 • Registration Fee: Hii inatozwa 20% ya kodi ya ardhi ya mwaka(Annual Land Rent) Mfano kodi ya mwaka ya kiwanja ni 20,000/=, RF=20,000/= X 0.2=4000/=
 • Survey Fees: Hii hutegemea na hamashauri husika
 • Certificate of Preparation: 50,000/=
 • Deed Plan Fee: 20,000/=
 • Stamp Duty : (land rent-2,000)50/1000=290

4. Utatakiwa pia awasilishe Picha Sita za Pasipoti Saizi za Rangi za hivi karibuni.

Kwa Maeneo Ya Kijijini Yaliyo Chini Ya Sheria Ya Vijiji

Hatua hizi ni kwa wawekezaji wenye Mashamba makubwa

1. Kuwasilisha ombi la kutaka kupimiwa ardhi ya shamba lako kwa Halmashauri ya Kijiji husika.

2. Kujadiliwa ombi lako la kutaka kupima shamba na Halmashauri ya Kijiji husika.

3. Halmashauri ya Kijiji husika wataandika muhtasari iwapo watakuwa wamekubali ombi hilo.

4. Halmashauri ya Kijiji husika itaitisha Mkutano Mkuu wa Wanakijiji wote ili kujadili ombi hilo la kutaka kuhawilisha ardhi hiyo.

5. Wanakijiji wakiridhia ombi hilo la kuhawilisha ardhi, Mwenye Shamba ataandika barua yenye kuambatana na mihtsari yote miwili kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, kuomba kuhawilisha shamba lake.

6. Mkurugenzi Mtendaji Wilaya akiridhia, Mwenye Shamba atatakiwa kuhakikisha kuwa Afisa Ardhi Mteule Wilaya na Mkuu wa Wilaya wanafika katika kijiji husika na kufanya Mkutano Mkuu wa Hadhara wa Wanakijiji wote     ili kujiridhisha na maombi haayo ya kuhawilisha ardhi.

7. Wanakijiji wakiridhia uhawilishaji huo wa ardhi mbele ya Mkuu wa Wilaya na Afisa Ardhi Mteule Wilaya, Afisa Ardhi Mteule ataandika barua kwenda kwa Waziri wa Ardhi ili kumtaarifu kuhusu ombi hilo la uhawalishaji         wa ardhi.

8. Waziri wa Ardhi akikubali uhawilishaji huo wa ardhi, Mwenye Shamba ataandika tangazo la kusudio la kuhawilisha ardhi hiyo na kuliweka kwenye shamba husika kwa muda wa siku 90.

9. Kama hakuna pingamizi lolote litakalotolewa na mtu yeyote, taratibu za kuhawailisha shamba hilo zitaendelea kwa mujibu wa sheria za ardhi.

10. Atatakiwa kulipia gharama za mchoro wa mipango miji na gharama za soroveya.

11. Atatakiwa kulipia gharamza za mchoro wa mipango miji na soroveya kuwasilishwa Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kupitishwa.

12. Atatakiwa kulipa gharama za kuandaliwa hati miliki ambazo ni Primiamu, Ada ya Maombi ya Kiwanja, Ada ya Soroveya, Gharama ya Malipo ya Ramani kwa Ajili ya Kuandaliwa Hati, Malipo ya Hati, Malipo ya Stampu,       Malipo ya Kodi ya Ardhi na Malipo ya Usajili wa Kiwanja husika.

13. Baada ya kukamilika kwa malipo hayo yote, atatakiwa kuwasilisha Kitambulisho chochote kinachokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi kama vile Nida, Mpiga Kura, Cheti cha Kuzaliwa n.k.

14. Atatakiwa pia awasilishe Picha Sita za Pasipoti Saizi za Rangi za hivi karibuni.

Vitu 8 Muhimu Vya Kuwa Navyo Ili Uweze Kupata Hati Miliki Ya Kiwanja/Shamba Lako

1. Ramani Ya Upimaji,

Eneo husika lazima liwe na ramani ya upimaji ambayo imeizinishwa na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, iwe na mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa ramani na upimaji.

2. Ramani Ya Mipango Miji

Eneo husika lazima liwe ramani ya mipango miji yenye kuonyesha matumizi husika ya eneo lako. Lazima iwe imeizinishwa na wizara na ina mhuri na sahihi ya mkurugenzi wa mipango miji.

3. Mkataba Wa Umiliki

Lazima uwe na mkataba wa umiliki wa eneo lako, kama ulinununa, ulipewa zawadi, ulirithi n.k, Uwe na mhuri wa mwanasheria.

4. Fomu Ya Mipaka (Land Form. 92)

Lazima uwe na fomu ya mipaka ambayo itaonyesha majirani unaopakana nao pande zote wakisaini kukubaliana na mipaka, itasainiwa pia na viongozi wa serikali yako ya mtaa.

5. Fomu Ya Maombi Ya Hati (Land Form. 19)

Fomu kwa ajili ya maombi ya hati, unajaza taarifa zako mfano jina, anuani, sahihi n.k

Join The Discussion

One thought on “Hatua na Jinsi ya Kupata Hati Miliki Ya Kiwanja 2022”

 • Moses ndimbo

  Keep working, we understand you.

  Reply
 • Willfred laizer

  Mimi ni mkazi wa Arusha Kijiji Cha oldada nilitaka kujua garama za upimaji wa ardhi na kupata hati miliki 0677808408

  Reply
 • Nasibu mbiro

  Mm nipo dar wilaya ya ilala kata ya majohe
  nauriza garama yake jumla
  Shingapi

  Na ili upimiwe na upate namba ya nyumba una fanyaje

  Reply
 • Willy Sanga

  Tunaomba namba husika ili tuweze kupiga simu tujulishane mengi Zaid kuusu hati miliki

  Reply

Compare listings

Compare
Search
Price Range From To